Jumatano 22 Oktoba 2025 - 07:30
Vipengele vitatu muhimu kwa ajili ya kazi ya kitamaduni / Tuwe tayari kufanya biashara na Mungu

Hawza/ Mkurugenzi wa hawza Iran, Ayatullah Alireza A‘rafi, akifafanua kuhusu vipengele vitatu muhimu vya kazi ya kitamaduni, alisema: “Ikhlasi ni kipimo kinachoinua thamani ya kazi. Kufanya biashara na Mungu huzalisha ladha na baraka zisizopatikana popote pengine. Katika kila hatua, tunapaswa kuwa tauari kufanya biashara na Mungu.”

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah A‘rafi — Mkurugenzi wa hawza — katika mkutano wa 93 na manaibu wa utamaduni na wakuu wa taasisi na vituo vya kitamaduni vya Jihad-e-Daneshgahi uliofanyika kwenye ukumbi wa Shahid Ahmadi-Roshan wa Chuo Kikuu cha Qom Iran, alisisitiza umuhimu wa kazi za kitamaduni akisema:
"Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika aya ya 108 ya Sura Yusuf":


{ قُل هَـٰذِهِۦ سَبِیلِی أَدۡعوا۟ إِلَى ٱللَّهِۚ عَلَىٰ بَصِیرَةٍ أَنَا وَمَنِ ٱتَّبَعَنِی وَسُبحَـنَ ٱللَّهِ وَمَا أَنَا مِنَ ٱلمشر كِینَ}

“Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua - mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina.”
[Surah Yūsuf: 108]

Akasema kuwa aya hii inaashiria mambo muhimu ambayo ni kipimo cha kwanza cha kazi ya kitamaduni katika njia ya risala ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w.).

Vipengele vitatu muhimu kwa ajili ya kazi ya kitamaduni

Kipengele cha kwanza: Kazi ya kitamaduni ielekezwe kwenye ulimwengu wa kiroho.

A‘rafi alisema: “Kipengele cha kwanza katika njia ya utume ni ‘kulingania kwa Mwenyezi Mungu’. Hii inaonesha kwamba asili ya mwanadamu siyo mali wala mambo ya kimwili pekee; bali kila kitu kinapaswa kuelekezwa kwenye upeo wa juu zaidi wa maisha bora ya kiroho. Kwa hiyo, sifa ya kwanza ni kwamba kazi ya kitamaduni lazima iwe imeelekezwa kwenye ulimwengu wa kiroho, ambapo nuru ya Mungu imeenea. Mungu ndiye lengo kuu la maisha, na Yeye ndiye motisha inayotuwezesha kuendelea katika jihad na harakati.”

Kipengele cha pili: Basira na ufahamu wa njia

Akaongeza: “Njia hii inaendelea kwa ufahamu na maarifa ya kina kuhusu mwelekeo na kila kitu kilicho njiani. Mtume (s.a.w.w.) hakuongoza tu kuielekea haki, bali pia alifundisha mbinu bora na za hekima. Kwa hiyo, njia hii lazima ipitiwe kwa basira.

Kipengele cha tatu: Mtandao wa kitamaduni na mfumo wa kifikra

A‘rafi alisema: “Kipengele cha tatu katika msafara wa uongofu wa Mtume na kila kazi ya kitamaduni ni kwamba njia hii huwezi kuipita peke yako. Inahitaji kundi, mtandao wa kitamaduni na mfumo wa fikra. Mfumo huu hauishii katika kiwango cha tukio la Ashura tu, bali unapanuka zaidi.”

Akaendelea kusena: “Lolote tutakalosema kumhusu Mwenyezi Mungu ni dogo mbele ya ukuu Wake, kwa kuwa akili zetu haziwezi kuifikia heshima Yake. Udhaifu wa hisia na mapenzi yetu mbele ya Mungu na rehema Zake uko wazi. Hivi vipengele vitatu ndizo nguzo za njia ambayo Mtume alisema: ‘Hii ndio njia yangu.’”

Tuwe tayari kufanya biashara na Mungu

Ayatullah A‘rafi alisisitiza: “Ikhlasi ndicho kipengele kinachoinua thamani ya kazi. Kufanya biashara na Mungu kunazaa ladha na baraka ambazo hazipatikani mahali pengine popote. Katika kila jambo tunalolifanya, tunapaswa kuwa mezani kwa ajili ya kufanya biashara na Mungu.”

Aliendelea kusema: “Tupo katika zama ambazo sura ya dunia imetengenezwa na fikra za ustaarabu wa Magharibi. Ustaarabu huu una faida ambazo haziwezi kupuuzwa, lakini pia unahusisha mitazamo na mawazo yaliyo mbali na mtazamo wetu wa kiimani. Mtazamo huu umeenea katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu, na kwa hivyo ni lazima tuutazame kwa uadilifu, lakini pia tuukosoe kwa busara.”

Umuhimu wa nadharia za kati kwa ajili ya kujibu maswali ya vijana

Mkurugenzi wa hawza aliongeza kuwa: “Nadharia za kati (nadharia zinazounganisha dini na sayansi au dini na jamii) zina umuhimu mkubwa katika kujibu maswali ya kizazi cha vijana.

Tofauti kati ya Shahīd Murtadhā Muttahari na wengine ilikuwa ni kwamba; yeye aliweza kuchimba kutoka katika hazina za kielimu na kidini, nadharia zilizokuwa zikielezea akili za watu na kujibu maswali yao ya msingi kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Taasisi za kitamaduni, mbali na kazi za kielimu na za msingi, zinapaswa kuzalisha na kuwasilisha nadharia hizi za kati. Hii ni kazi kubwa ambayo bado tuna mapungufu ndani yake na inapaswa kupewa kipaumbele.”

Mchanganyiko wa elimu, hamasa na imani

Akaendelea kusema: “Kazi ya kielimu na kiutamaduni, mbali na akili, uwezo wa kifikra na mpangilio mzuri, inahitaji pia hamasa na hisia sahihi. Mchanganyiko huu wa hisia na elimu ni muhimu mno katika kutekeleza majukumu na kufanikisha malengo, kwani una athari kubwa isiyoweza kupingwa.”

Mwisho, alikumbusha kuwa taasisi ya Jihad-e-Daneshgahi ni taasisi iliyozaliwa kutoka katika moyo wa Mapinduzi ya Kiislamu na imeota mizizi ndani ya watu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha